Saturday, 5 April 2014

Unajua inachukua hatua gani za kibaolojia hadi inafikia unatoa hewa chafu (kutoa ushuzi)!? Fuatilia hapa.

Kamusi ya Kiswahili Sanifu huita tendo hili kuwa ni, kujamba, sura au ushuzi, lakini kwa lugha isiyo na makali, huitwa kutoa hewa
chafu.

Pamoja na jamii kuchukulia tendo hilo la kutoa hewa chafu kama la aibu na unapolifanya mbele ya watu huweza kumfanya mtu asijisikie vizuri,  lakini  yapo mengi ya kibaolojia yanayofanyika hadi binadamu akatoa hewa chafu mwilini.

Kwa kifupi huu ni mfumo halisi na wa kila siku wa utendaji kazi wa miili yetu ndiyo husababisha hali hii.

Daktari bingwa wa magonjwa ya ndani ya mwili,  Meshack Shimwela anasema kutoa hewa
chafu kunasababishwa na kubanwa kwa hewa ambayo tunaipata au kuimeza wakati wa kula au kunywa.

Pia, hewa chafu huweza kuingia kutokana na gesi kuingia kwenye utumbo kutoka kwenye damu. Gesi hizi huweza kuzalishwa na kemikali katika utumbo au bakteria.

Dk. Shimwela anasema bakteria wanaoishi tumboni, humeng’enya chakula na kuzalisha gesi ya ammonia, sulfur dioxide ambazo huwa na harufu mithili ya choo au mkojo. “Harufu hutegemea aina ya chakula. Tumbo lenyewe,
likipata maradhi au maambukizi huongeza kasi ya gesi,” anasema

Anaongeza kuwa bakteria wabaya wanaweza kutengeneza gesi na kuwa hewa chafu ikizidi sana ni tatizo na inaashiria tatizo.

Chanzo:Mwananchi