Watu watatu akiwamo mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Calvin Saleka (23) wamekamatwa naJeshi la Polisi mkoani Dodoma kwa tuhuma za kupatikana na bangi kilo 133.5 yenye thamani ya sh milioni 20.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, David Misime, alisema jana kuwa mwanafunzi huyo wa mwaka wa pili alikamatwa na mabegi mawili yenye uzito wa kilo 51.
Mbali na mwanafunzi huyo, mwingine aliyekamatwa ni John Joseph (31), mkazi wa Kinondoni, Dar es Salaam ambaye alikamatwa akiwa na mabegi mawili yenye bangi yenye uzito wa kilo 42 na
Joseph Batoni, mkazi wa Shinyanga
alikamatwa na mabegi mawili yenye uzito wa kilo 36.
Kamanda Misime alisema watu hao
walikamatwa katika stendi kuu ya
mabasi mjini hapa baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia mwema.
Alisema watuhumiwa hao walikuwa
wamepanda basi kutoka Kijiji cha
Manonga-Tinde, mkoani Shinyanga
kwenda jijini Dar es Salaam.
“Waliweka bangi hiyo katika mabegi
makubwa ya nguo na kufunga kwa
nailoni kisha kusaga vitunguu na kuweka katika begi hizo pamoja na kupulizia manukato (perfume) ili kuondoa harufu
ya bangi,” alisema.