Habari ambazo zimetufikia hivi punde ni kwamba yule shemeji wa wana Bongo Movie na walimbwende hapa nchini Papaa Sunday Demonte ambaye alimuoa Aunt Ezekiel yupo sero hivi sasa katika moja ya viunga vya dola vya
Dubai.
Taarifa hii kutoka chanzo chetu cha
uhakika cha karibu na Pendeshee huyu wa magari kutoka huko Dubai zinasema Pendeshee
huyu amekamatwa kwa madai mbalimbali likiwemo la kuto kuishi kihalali katika Nchi hiyo kwa kipindi kirefu ambayo nimaarufu kwa biashara duniani.
Kwa mujibu wa chanzo chetu Papaa huyu alikuwa akisakwa muda mrefu sana, ata wakati
anafunga ndoa na Aunt Ezekiel alikuwa akiishi kimashaka mashaka kwa kuogopa kuingia katika mikono ya dola ya waarabu hao.
Mtandao huu umejitahidi kumtafuta Aunt Ezekiel ili
kumuuliza kama taarifa hizi anazo, ila simu yake haikupatikana mpaka tunaingia mitamboni, vile
vile mtandao wako unajaribu kuwasiliana na mwakilishi wetu wa serikali nchini humo Bwana
Omary Mjenga ili kuweza kujua kama wana taarifa yoyote ya kukamatwa kwa mtanzania
huyu na nini wanatakiwa kufanya ili kuweza kujua chanzo kikuu na nini hatua ambazo zinatakiwa kufuatwa za kuweza kumsaidia.