Sunday, 6 April 2014

Kifaa cha kupimia UKIMWI chauzwa kwa watu binafsi Uingereza.

Serikali ya Uingereza imepitisha sheria inayoruhusu uuzaji wa kifaa cha kupimia virusi vya ukimwi kwa watu binafsi ili kuwawezesha
kujifanyia vipimo vya ukimwi wawapo majumbani kwao.

Serikali hiyo ilikuwa imeruhusu ufanyaji wa vipimo vya ukimwi majumbani tangu September
mwaka jana lakini sheria rasmi imeanza kufanya kazi Jumapili hii.

Hata hivyo, vifaa hivyo ambavyo vitakuwa vinafanya kazi kwa kuchukua tone dogo la damu
kwenye kidole cha mhusika havipo Uingereza kwa sasa, lakini kituo cha Terrence Higgins Trust HIV
Charity kimesema kuwa majaribio ya kifaa hicho yanaweza kuanza nchini humo mwaka huu au
mwanzoni mwa mwaka 2015.

Imeripotiwa kuwa kuwepo kwa kipimo hicho kutasaidia idadi inayokadiriwa kuwa wananchi
zaidi ya 25,000 wanaoishi na VVU lakini bado hawajapimwa na wataweza kufahamu afya zao
kirahisi.

Chanzo: Timesfm Tz