Pakkirappa Hunagundi ni mjenzi wa kihindi ambaye amezoea kula matofali na ni jambo ambalo anashindwa kuliacha kwa kuwa ameshazoea
Pakkirappa mwenye umri wa miaka 30 alianza kula matofali na vitu kama hivyo tangu alipokuwa na miaka 10.
Kwa miaka 20 sasa amekuwa akila vitu kama udongo wa matofali kilo 3 kwa siku.
Licha ya maajabu yote haya anayoyafanya, hajawahi kupata ugonjwa wowote, alisema.
Na anapanga kutumia uwezo wake huo kujipatia kipato kwa kufanya maonyesho sehemu mbalimbali nchini India.