Jamaa mmoja ameachwa bila sehemu zake za siri baada ya kuruhusu ziliwe na mnyama mwenye uchu kuliko wote, Fisi, kwa kile alichodai kuwa angepata utajiri.
Chamangeni Zulu, kutoka: Malawi alisema kuwa, aliamua kufanya hivyo kwa sababu alipata ushauri kutoka kwa mganga wa kienyeji kuwa akipoteza sehemu zake za siri kwa kuliwa na fisi basi angepata utajiri.
Baada ya kupata ushauri huo Zulu alikwenda msituni moja kwa moja na kumwachia fisi atafune baadhi ya viungo vya mwili zikiweno sehemu zake za siri.
Alisema kuwa Fisi huyo alianza kutafuna baathi ya vidole vyake vya mkononi na baadae kumalizia na nyeti.
Alifikishwa hospitali kwa matibabu baada ya kugunduliwa na polisi huko msituni. Hata hivyo, Zulu bado anatumai kuwa atapata utajiri kwa kuwa ameshatimiza mashariti ya mganga.
Umasikini nao!!!