Imetokea huko Afrika kusini ambako jamaa mmoja, 24, anashikiliwa na polisi akihusishwa na mauaji ya aliyekuwa mpenzi wake, 21, ambaye alikuwa mjamzito kwa kumchoma moto na kumkatakata vipande.
Inasemwa na polisi kuwa, jamaa huyo mkazi wa Chesterville aliyatambua mabaki yanayoaminika kuwa ni mabaki ya aliyekuwa mpenzi wake aliyeripotiwa kupotea tarehe 21 februari 2014.
Polisi ilisema kuwa, inaaminika kuwa dada huyo aliyekuwa mjamzito alichomwa moto na kukatwakatwa vipande baada ya kuchomwa na kitu kizito kichwani; na uchunguzi kugundua kama mabaki ndio yenyewe ama la unafanyika.
Jambo la ajabu, jamaa huyo nwanzoni alikataa madai ya kufahamu mahali alipokuwepo mpenzi wake ila baadae alisema kuwa alimsindikiza kituo cha gari kwa kuwa alikuwa anataka kwenda hospitali.
Uchunguzi kufahamu sababu ya mauaji bado unaendelea, na kuna uwezekano kuwa jamaa akashtakiwa kwa kusababisha vifo vya watu wawili, mama na mtoto.