Watu 2 wameuawa na wengine 10 kujeruhiwa baada ya mtu mmoja aliyejihami kwa bunduki kuwafyatulia risasi
ndani ya kanisa karibu na mji wa bandari ya Mombasa nchini Kenya.
Maafisa wa polisi katika wilaya ya Likoni ambayo iko kusini mwa Mombasa wamesema kuwa
majambazi hao walilivamia kanisa hilo na kuanza kuwafyatulia risasi waumini hao kiholela.
Usalama umeimarishwa katika eneo hilo kufuatia kutiwa mbaroni kwa watu wawili siku ya jumatatu
ambao polisi wanadai walikuwa wakimiliki mabomu yaliofichwa ndani ya gari yao.
kumekuwa na visa tofauti vya ghasia mjini Mombasa katika miezi ya hivi karibuni vinavyoshirikisha vikosi vya usalama na waislamu
wenye itikadi kali.