Monday, 31 March 2014

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma asema haoni haja ya kurudisha fedha za umma zililizotumika kukarabati makazi yake. Twende tukapate mengi na vitendo.

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema hadhani ni sawa kurejesha fedha za umma
zilizotumiwa kukarabati nyumba yake binafsi kwa sababu hakuwahi kutoa pendekezo hilo.

Bw. Zuma amesema haoni haja ya kuchangia pesa zake binafsi katika ukarabati wa nyumba hiyo
kwani halikuwa pendekezo lake toka mwanzoni.

Pis, bwana Zuma amekiambia kituo kimoja cha Tv nchini Afrika Kusini kwamba maafisa wa serikali ndio waliopanga ukarabati huo uliogharimu dola milioni 23 bila kumuarifu.

Hii ndio mara ya kwanza Rais Zuma
amezungumzia kuhusu makazi hayo yaliyozua mjadala mkali wa umma Afrika Kusini.

Mhifadhi wa mali ya umma alisema baadhi ya ukarabati uliofanywa sio halali na kumtaka Zuma kurejesha baadhi ya fedha zilizotumika.