Popo hutumiwa kutengeza kitoweo maarufu sana katika baadhi ya maeneo ya nchi ya Guinea.
Lakini kwa sasa inahofiwa kuwa popo wanachangia kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola kusini mwa nchi hiyo.
Nchi ya Guinea ni marufuku kwa kula na kuuza popo, na maafisa nchini humo sasa wamepiga marufuku uuzaji na ulaji wa nyama ya popo.
Hii katika juhudi za kudhibiti ugonjwa hatari wa Ebola, ambao kufikia sasa umesababisha vifo vya watu 62.
Nchi za kanda hiyo zikiwemo Liberia na Sierra Leone, zimechukua hatua kabambe kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa huo.
Hatua hizo zikiwemo kuwafanyia uchunguzi wa kiafya watu wanaongia mipakani.
Maafisa wa afya wanapata msaada kutoka shirika la afya duniani na ujumbe wa kuhamasisha watu
unapeperushwa kupitia televisheni.
Watu watano kati ya sita walioingia nchini Liberia kutoka Guinea walikua na ishara za ugonjwa huo na wamethibitishwa kufariki.
Hata hivyo maafisa wa utawala nchini Liberia bado hawajathibitisha kikamilifu kama kweli walikufa kutokana na ugonjwa wa Ebola.