Saturday, 22 March 2014

Hammer Q awaomboleza 5 Star. Twende sote hapa na vitendo kufahamu mengi zaidi.

Msanii wa muziki wa taarabu na
mduara nchini, Hussein Mohammed ‘Hammer Q’ juzi aliomboleza  miaka mitatu tangu msiba wa wanamuziki 13
wa bendi ya 5 Star, waliofariki dunia kwa ajari ya gari Machi 21, mwaka 2011, Mikumi, Morogoro.

Hammer Q kupitia kurasa zake za
mitandao ya kijamii; instagram na
facebook, aliandika ujumbe mzito
akiwakumbuka wenzake akisema kila Machi 21, amekuwa akikumbuka siku hiyo ya huzuni kubwa iliyowapoteza wasanii hao kwa mpigo.

“Kila inapofika tarehe kama ya leo
(Machi 21), moyo wangu huumia sana na hukosa furaha kabisa. Ni siku niliyopoteza rafiki /ndugu zangu 13 katika ajali ya gari iliyotokea Mikumi, Morgoro, tukiwa safarini kurejea Dar es Salaam,” anasema.

“Nilishuka njiani kwa ajili ya shughuli nyingine, baada ya muda nikapata simu ya kuniarifu wenzangu wamepata ajali na wamefariki dunia, dah nilidata kwa
kweli ule mshtuko niloupata siku ile, kila inapofika tarehe ya leo, hua napatwa na mshtuko wa aina yake nikirejea katika tukio,” alisema na kuongeza:

“Kazi yake Mola haina makosa, mbeleyao nyuma yetu, Mungu awalaze mahala pema peponi. Amin,” aliandika Hammer Q huku watu mbalimbali wakiungana
naye katika kuomboleza wakimpa pole na kuwaombea wote waliotangulia mbele za haki.