Thursday, 20 March 2014

Aishi na risasi kichwani kwa miaka 48 bila shaka, daaa!. Ebu mfuate vitendo hapa upate kionjo cha maajabu haya.

Mama mmoja amefanyiwa upasuaji wa kichwa ili kuondoa risasi iliyokuwa imekwama kwa miaka 48 kwenye fuvu lake kichwani ambayo inasemekana iliingia wakati yupo mtoto.

Mama huyo alijulikana kwa jina la Zhao aligindulika ana risasi kichwani kwake alipokwenda hospitali kupata matibabu ya maumivu ya kichwa ndipo madaktari wakagundua alikuwa na risasi kichwani.

Risasi hiyo ilikuwa na urefu wa 2.5cm na upana wa 0.5cm ambayo ilikuwa imejificha kwenye fuvu la kichwa chake na kufanikiwa kuitoa katika hospitali ya China Medical University.

Zhao alisema kuwa anafuhari kuwa risasi hiyo haikumuua na anashangaa jinsi gani na wakati gani risasi hiyo iliingia. Anasema pia, anahisi iliingia wakati huo alpohisi amegongwa na kitu kama jiwe kichwani na kukipotezea.