Rais wa Nigeria Goodluck Jonathana ameagiza shule zote na ofisi za serikali katika mji mkuu wa Abuja nchini humo zifungwe wakati wa siku tatu za Mkutano wa Uchumi wa Dunia World Economic Forum utakaanza nchini humo jumatano ijayo.
Serikali imesema hatua hiyo ni kuarahisisha misafara ya magari. Lakini suala la kuimarisha ulinzi huenda ni mambo yaliyosababisha hatua hiyo.
Ulinzi mkali umehaidiwa kwa wageni wapatao 1000 wakati wa mkutano huo.
Rais Jonathan amesema polisi wapatao 5000 na wanajeshi watafanya doria na kushika hatamu za ulinzi wakati wa mkutano huo utakaoanza wiki ijayo.
Waziri Mkuu wa China Li Keqiang na Marais wa Rwanda, Senegal na Kenya ni miongoni mwa viongozi wa juu wa nchi watakaohudhuria.
Rais wa Nigeria