Tuesday, 17 May 2016

Rasmi: Hakuna Costa, Mata, Torres katika kikosi cha Hispania Euro 2016

Wachezaji maarufu kadhaa wa Hispania, wengi kutoka Ligi ya Kuu ya Uingereza, waliachwa nje ya kikosi cha timu ya taifa cha wachezaji 25 cha kocha Vicente del Bosque kwa michuano ya Ulaya nchini Ufaransa.

Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, mshambuliaji wa Atletico Madrid Fernando Torres, kiungo wa Manchester United Juan Mata na nyota wawili wa Arsenal Santi Cazorla na Hector Bellerin wote hawapatikani kwenye orodha ya del Bosque.

Hapa kuna orodha kamili ya kikosi, ambayo inakuwa na wachezaji watano tu wa Ligi Kuuya Uingereza: David de Gea, Cesar Azpilicueta, David Silva, Cesc Fabregas na Pedro Rodriguez.

Sokkaa kupitia Goal.com