Friday, 20 May 2016

Ozil atamba Arsenal na tuzo ya msimu

Mesut Ozil ameshinda tuzo ya Mchezaji bora wa Msimu katika Arsenal baada kuandika rekodi ya kumaliza msimu akiwa na pasi saidizi nyingi katika Ligi Kuu ya Uingereza.

Mjerumani wa kimataifa amewashinda wenzake kama vile Alexis Sanchez, ambaye amepata nafasi ya pili, na HectorBellerin, ambaye ameshikilia nafasi ya tatu, akiwa na kura nyingi kutoka kwa mashabiki.

Ozil alifunga mabao sita na kutoa pasi saidizi 19 katika Ligi Kuu ya England na kusaidia Arsenal kumaliza msimu wakiwambele ya mahasimu wao wa jadiTottenham kutoka North London.