Tuesday, 24 May 2016

Nuh mziwanda adai kuwa uhusiano na Shilole umemletea majanga

Nuh Mziwanda amedai katika miaka mitatu aliyokuwa na uhusiano na Shilole amepoteza mambo mengi.

Akiongea na Bongo5 Nuh amesema hakuna zaidi anachokumbuka kwenyeuhusiano huo zaidi ya majuto.

“Kuna vitu muhimu sana ambavyo nimegundua ningeweza kuvifanya na ningekuwa nipo mbali sana,” amesema Nuh. Muimbaji huyo amesema uhusiano huo ulimfanya auchukulie poa muziki na hivyo kushindwa kutengeneza hit song.Anasema Shilole alihakikisha katika muda wote waliokuwa nao Nuh asihit kwa uoga kuwa akiwa staa atamuacha.

“Yule [Shilole] alikuwa na trick nyingi za kunifanya mimi nijionee staa tayari, nijione mimi napendwa na watu au mimi muziki wangu unavumakumbe bado halafu yeye huku muziki wake unaenda,” amesisitiza.

Bongo5.com