Tuesday, 24 May 2016

Hatima ya Ryan Giggs Old Trafford baada ya LVG kufukuzwa

Manchester United waripotiwa kwamba wamempa Ryan Giggs nafasi ya kuendelea kukaa katika Old Trafford kabla ya meneja mpya anayetarajiwa kuchukua madaraka, kwa mujibuwa Manchester Evening News.

Legendi wa United mwenye mafanikio zaidi katika klabu na mwenye kuwa na michezo mingi yaripotiwa kwamba alijulishwa na klabu Jumatatu mchana kuwa ataendelea kukaa katika Old Trafford.

Mwelisi alikuwa meneja msaidiziwa Louis van Gaal kwa kipindi cha misimu miwili, baada ya kuhudumu kama kocha-mchezajichini ya umenejimenti wa David Moyes kabla ya kustaafu kwake kama mchezaji mnamo 2014.