Wednesday, 26 November 2014

Victor Wanyama aibiwa mali zake

Maafisa wa polisi wanachunguza kisa kimoja ambapo wezi walivunja na kuingia katika nyumba ya mchezaji wa kilabu ya Southampton Victor Mugubi Wanyama nchini Uingereza na kumuibia mali yake usiku wa jumatatu.

Shati moja la kiungo wa kati wa timu ya Barcelona Andres Iniesta ,pamoja na nguo za wanamitindo kadhaa pamoja na jozi 20 za viatu ni miongoni ya vitu vilivyoibwa.

Wezi hao pia waliiba gari la mchezaji huyo aina ya Land Rover lenye thamani ya shilingi millioni 8.4 fedha za kenya,fanicha,Runinga pamoja na vifaa vyengine vya kielektroniki .

Mkenya huyo mwenye umri wa miaka 23 anaishi katika nyumba ndogo na polisi wameshangazwa kwamba majirani zake hawakuamshwa na kelele za uvunjaji huo.