Tuesday, 25 November 2014

Umeipata hii ya wanafunzi kufanyishwa vibarua na waalimu wao ili kupata fedha ya kununulia chaki?

Wananchi wa kijiji cha Karukekere wilayani Bunda, mkoani Mara, wamelalamikia kitendo cha wanafunzi wa Shule ya Msingi Karukekere, kudaiwa kufanyishwa kazi za vibarua vya kulima na kazi nyingine na walimu wa shule hiyo.

Wanafanyishwa kazi hiyo ili wapate fedha za kununua chaki wakati wa vipindi vya masomo.

Walitoa kero hiyo juzi kwenye mkutano wa hadhara kijijini hapo, ambao ulihutubiwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Boniface Mwita na Mwenyekiti wa CCM wilayani Bunda, Chacha Gimanwa, waliokuwa wakihamasisha wananchi kujiandikisha kwa ajili ya kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Picha sio halisi