Friday, 28 November 2014

Tibaijuka: nimechukuwa fedha za escrow kama mchango wa shule

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka amesema kuwa alipokea fedha za Escrow kama mchango wa shule ambao aliuomba kutoka kwa Mmiliki wa Kampuni ya VIP Engineering and Marketing, James Rugemalira.

Amesema kwamba aliipokea fedha hizo kiasi cha bilioni 1.6 bila kujua kama ni fedha zilizotoka kwenye akaunti ya escrow na kuzipeleka kwenye undelezaji wa shule ya sekondari Barbro Johansson kama ufadhili wa shule.

Mjadala kuhusu kashfa ya uchotaji wa mamilioni ya fedha katika akaunti ya ESCROW ya Benki Kuu ya Tanzania umezidi kuunguruma  kufuatia taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, PAC, na ripoti ya serikali kuhusu kashafa hiyo.