Saturday, 22 November 2014

Lionely Messi avunja rekodi ufungaji La Liga kwa namna ya pekee

Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi amefanikiwa kuibadilisha historia ya ufungaji wa wakati wote kwenye ligi kuu ya hispania maarufu kama La Liga.

Messi alivunja rekodi ya Telmo Zarra aliyekuwa na magoli 251 kwa kushinda magoli 3 (hat-trick) dhidi ya Sevilla ambayo yalimfanya Messi kuwa na magori 253.

Messi aliingia uwanjani dhidi ya Sevilla jana akihitaji goli moja tu kuifunika rekodi ya aliyekuwa mchezaji wa Athletic Bilbao, Telmo Zarra na alifanikiwa pindi alipofunga goli la mpira wa adhabu kipindi cha kwanza.

Messi aliendelea kuandika rekodi ya tofauti baada ya kufunga goli la 252 kipindi cha pili. Messi aliongeza goli la tatu na kutimiza goli la 253.