Thursday, 13 November 2014

Lipate hili walilolifanya wananchi hawa, je wapo sahihi?

Wafanyabiashara katika Soko la Sido jijini Mbeya, juzi waligoma kulipa ushuru, wakishinikiza kwanza halmashauri ya jiji kuondoa taka.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wafanyabiashara hao walisema wamelazimika kuchukua hatua hiyo baada ya wahusika kushindwa kuzoa takataka kwa miezi sita sasa.

Lucia Siwinga na Hadija Tawila, wafanyabiashara wa eneo hilo, walisema wamesitisha kukusanya kodi za halmashauri ya Jiji ili liondoe takataka kwanza.

Walisema wameamua kusitisha ukusanyaji wa kodi za halmashauri ya Jiji kwa sababu wanachukua ushuru, lakini hawatatui matatizo ya uchafu.

Kwa upande wake, mwenyekiti wa usafi sokoni hapo, Philiston Mwasomola ambaye pia ni mjumbe wa soko, alisema wiki tatu zilizopita walikuja wanasheria wa halmashauri ya jiji na waliahidi kuondoa takataka hizo.

Kaimu mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Wenceslans Lindi alisema walipata malalamiko yao na walipeleka gari binafsi kwa ajili ya kuondoa takataka hizo.

“Tulikaa mezani baada ya kupata malalamiko yao, hivyo tumepeleka gari binafsi kuzoa takataka hizo,” alisema Lindi.

Via Mwananchi