Kwa mara nyingine Chelsea imeonyesha ni moto wa kuotea mbali baada ya kuifunga Liverpool 2 - 1 mbele ya mashabiki wao katika uwanja wa Anfield.
Liverpool ndio waliokuwa wa kwanza kufunga goli lililotiwa wavuni na Emre Can baada ya kupiga shuti na kumgonga beki mmoja wa Chelsea na kujaa wavuni.
Baadae Chelsea wakaja juu na kusawazisha goli kupitia kwa Gary Cahill baada ya mlinda mlango wa Liverpool Simon Mignolet kuingia na mpira wavuni wakati alipokuwa ameudaka. Goli la pili la Chelsea lilifungwa na Diego Costa kwa shuti kali umbali wa takribani meta 15 ndani kisanduku cha 18.
Mechi hiyo ya Chelsea na Liverpool katika uwanja Anfiled kunarejesha kumbukumbu zisizofurahisha kwa upande wa Liverpool pamoja na hali yao ya baadaye ambayo si nzuri sana.