Mwanamke, Dionne Baxter, 24, amejikuta akiwekwa kovu la maisha kwenye titi lake la kushoto baada ya kuunguzwa na simu aina ya iPhone 4 aliyokuwa akiichaji.
Mwanamke huyo alichomeka simu hiyo kwenye chaji na kuilalia kwa kujisahau na pindi alipoamka alijikuta na mchilizi wa kuunguzwa titi lake tangu juu hadi chini ya titi.
Tukio la mwanamke Dionne Baxter kuunguzwa na simu aina ya iPhone ni mfulizo wa matukio yanayofanana ya watu kuunguzwa na simu za aina hiyo.