Wednesday, 21 May 2014

Man city wamfanyia ya kushangaza Yaya Toure kwenye siku yake ya kuzaliwa

Wakala wa kiungo wa Machester City, Yaya Toure amekashifu kupuuzwa kwa kiungo huyo kutoka Ivory Coast.

Dimitri Seluk alikashifu ujumbe wa kheri njema kwa Toure ambaye alikuwa anaadhimisha siku
kuu ya kutimiza miaka 31 mnamo mei tarehe 13.

Ujumbe huo ulioambatana na keki
haukumridhisha hata kidogo Seluk ambaye anasema kuwa alitarajia wamiliki wa klabu hiyo angalau kumtambua kiungo huyo wa Ivory
Coast, timu hiyo ilipotua Abu Dhabi
kusheherekea ushindi wao wa taji la Uingereza kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka mitatu.

Seluk alisema Toure huenda akaondoka iwapo wamiliki wa klabu hiyo wataendelea kumpuuza.

Toure alisaini mkataba mpya wa miaka minne mwaka uliopita licha ya Seluk ambaye amemuakilisha Toure kwa zaidi ya miaka kumi
kutishia kuwa kiungo huyo wa Ivory Coast angehama Etihad.

Uhusiano baina ya mchezaji huyo bora barani Afrika na Seluk umedumu kwa miaka mingi kiasi
ya kuwa Toure alimpa mwanawe wa pili jina la Seluk.

Via Bbcswahili