Friday, 16 May 2014

Achomwa moto kwa imani za ushirikina

Kitongoji cha Chanji Kisiwani Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa, Elizabeth Mwananjela, 60, ameungua na kufia ndani ya nyumba yake baada ya kuteketezwa na moto na watu wasiojulikana kisha kuibomoa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda alidai kuwa mkasa huo ulitokea Mei 14, mwaka huu sasa 5:00 usiku katika kitongoji hicho cha Chanji Kisiwani huku chanzo kikidaiwa kuwa ni imani za kishirikina.

Alisema siku hiyo ya tukio, mtu huyo alijeruhiwa na moto mwili mzima na kutolewa ndani ya nyumba yake hiyo ambamo alikuwa akiishi peke yake na kukimbizwa hospitali ya mkoa mjini hapa kwa matibabu. Lakini, alifariki dunia kabla ya kufika.

Mwaruanda alidai kuwa hakuna mtu yeyote hadi sasa aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

Alisema msako unaendelea ili kuwabaini wote waliohusika na uhalifu huo ili sheria iweze kuchukua mkondo.

Jacob Mwaruanda